Kazi ya usimikaji wa bomba (Draft tube) sehemu ya chini kabisa kwenye mashine nambari 9 inaendelea vizuri ambapo hatua hiyo imeanza Agosti 17, 2021, katika mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP).

Aidha bomba hizo katika mradi huo zitatumika kutolea maji katika mitambo ya kufua umeme na kuyarudisha mto Rufiji kwa ajili ya matumizi mengine.


Hata hivyo usimikaji wa mambomba hayo ni hatua kubwa iliyofikiwa baada ya kukamilika kwa uundwaji wa bomba hizi zinazofungwa katika kitako cha msingi wa zege, kilichopo eneo la mita 42.7 juu ya usawa wa bahari.


Usimikaji wa bomba hizi ndio utawezesha kuanza kwa ufungaji wa sehemu za juu za mashine (turbine) na kisha jenereta za kufua umeme.
Mkandarasi wa mradi huu ametokea Nchini Misri na mradi unatarajiwa kukamilika June 2022.

Waliojifanya Vishoka watiwa mbaroni
Luis Miquissone awaaga Msimbazi