Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alizaliwa  Oktoba 29, 1959 Wilayani Chato Mkoa wa Kagera ambayo hivi sasa ipo Mkoa wa Geita.

Harakati zake za kisiasa zilianza mwaka 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi. Mwaka 2000 Dk. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.

Aidha, katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi, na hatimaye katika uchaguzi wa mwaka 2015 Dk. Magufuli akachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leo Oktoba 5, 2016 Dk. John Pombe Magufuli anatimiza miezi 11 tangu ameapa kuwa Rais Novemba 5, 2015.

Rais Magufuli amekuwa mchapakazi na jasiri katika kipindi chote hadi sasa kwa kufanya maamuzi magumu bila kujali mtu, nafasi wala chama chake cha siasa, badala yake amekuja na ajenda ya kuwepo kwa nidhamu katika kufanya kazi ‘Hapa kazi tu’.

Rais Magufuli amedhamiria kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma kwa kutengua baadhi viongozi walioteuliwa na kufanya madudu na kuteua wengine ambao amewaona wanaendana na kasi yake ya utendaji kazi.

Magufuli ameweza kutengua uteuzi Waziri mmoja, Wakuu wa mikoa wanne, Katibu tawala wa mkoa na Wakurugenzi wawili wa Halmashauri.

Viongozi kadhaa wa umma walikula kiapo cha maadili ya utumishi wa umma baada ya kuteuliwa, huu ukiwa ni utaratibu mpya wa uongozi wa Rais Magufuli kwa lengo la kuwakumbusha kuwa utumishi wa umma unapaswa kuzingatia maadili.

“Tutahakikisha kwamba wanafunzi wengi zaidi wa elimu ya juu wanapata mikopo kwa wakati.  Tutashughulikia maslahi na kero za walimu wa ngazi zote ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu vijijini na kuiunga mkono Benki ya walimu ili iweze kuwanufaisha zaidi.” – Rais Magufuli

Mwanzoni mwa Januari, Rais Magufuli alianza kutekeleza ahadi yake ya kutoa elimu bure kwa ngazi ya elimu ya msingi na sekondari hadi kidato cha nne, Serikali ikisambaza fedha katika shule.

Machi 10, 2016 Rais Magufuli amefanya ziara ya kushitukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

Mpaka Rais Magufuli anatoa agizo hilo, Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini ya kufanyika malipo.

Mei  13, 2016 Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) na kuiagiza wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za kuondoa dosari iliyopo kwenye kitengo cha ukaguzi wa mizigo ya abiria.

Septemba, 26 2016 ametembelea Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo ambapo pamoja na mambo mengine ametoa miezi miwili kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kununua mashine nne za kukagulia mizigo bandarini (Scanning Mashine)

Mbali na ahadi mbali mbali ambazo Rais Magufuli anazitimiza, hivi karibuni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1), Dar es Salaam Rais Magufuli amezindua ndege mpya mbili za Serikali aina ya Bombardier Dash 8 Q400, ambapo ameitaka Bodi mpya ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kutosita kuwafukuza kazi wafanyakazi watakaobainika kuhujumu kampuni hiyo.

Aidha, ametangaza kuwa serikali imeanza mazungumzo ya kununua ndege nyingine mbili mpya, ikiwamo itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 240.

Pamoja na mambo mengine, katika muda wote wa miezi 11 hadi sasa Serikali imekuwa macho muda wote kutokana na jinsi Taasisi zote zinavyochapa kazi kwa umakini na uadilifu.

Amissi Tambwe: Sina Uadui Na Simba Hata Kidogo
Raymond: Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview