Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa kuna haja ya wabunge kuwaombea mawaziri kwenye mamlaka husika ili wapate fursa ya kusafiri nje ya nchi.

Ameyasema hayo mara baada ya hoja ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo amesema kuwa ni muhimu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage asafiri nje ya nchi, ili kujenga uhusiano wa Kidiplomasia na kutafuta masoko ya bidhaa za mbaazi, choroko na giligilani.

Aidha, Ndugai ambaye alikiri kukubaliana na mchango wa Zitto Kabwe amesema ni kweli mawaziri inabidi wasafiri na wabunge wanapaswa kuwaombea kutoka kwenye mamlaka husika.

“Waziri wa Biashara hawezi kukaa na sisi hapa, lazima aende, tumuombee popote pale kwenye mamlaka lazima asafiri, maana bidhaa zetu tutauza Kongwa, kuna soko huko, Waziri wa utalii lazima asafiri ‘apige mawingu’ huko na wengine huko, ndiyo ukweli jamani, sisi wabunge lazima tuwasemee,”amesema Ndugai

Eric Cantona kutua Old Trafford
Video: Maswali msamaha wa Mbunge Sugu, Babu atimiza azima ya kujiua