Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa Tanzania haikupiga magoti katika kipindi cha utawala wa awamu ya pili ilipokuwa na hali ngumu, hivyo haiwezi kufanya hivyo wakati huu ikiwa na hali nzuri zaidi

Amesema kuwa licha ya nchi kutokuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni wakati huo wa awamu ya pili (1985-1995), Tanzania haikupiga magoti kuomba msaada, lakini sasa Taifa lina akiba ya fedha za kigeni za miezi mitano

“Kama tuliweza kwa wakati huo hatuwezi kushindwa katika awamu hii ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, tumeamua kujitegemea na hili tunalitekeleza kikamilifu kwamba hatuwezi kupiga magoti kwaajili ya kuomba misaada.”amesema Prof. Kabudi

Profesa Kabudi aliyasema hayo Bunge jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja za Wabunge waliochangia mjadala wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Video: MO Dewji afunguka kutekwa kwake, Takukuru yanusa maficho ya bilionea
Wakuu wa mikoa waonywa kuhusu matamko wanayoyatoa