Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni ambaye pia ni Mbunge wa Babati Vijijini wamejiuzulu nafasi hizo, leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Ghasia na Soni, wametangaza uamuzi wao leo asubuhi mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jijini Dodoma na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amethibitisha kujiuzulu kwao.

“Ni kweli wamejiuzulu nafasi zao na mimi sijajua kwa nini wamejiuzulu,” amesema.

Bado haijafahamika sababu za viongozi hao kufanya uamuzi huo wa kujiuzulu.

 

Guedes atimka jumla Paris Saint-Germain (PSG)
Spika wa Bunge atishia kususia vikao