Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo Novemba 4, 2019 anawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni, akiwemo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Edwaed Kichere anayechukua nafasi ya Prof. Musa Assad ambaye kipindi chake cha mika 5 kimeisha.

Katarina Tengia, anaapishwa kuwa Katibu tawala mkoa wa Njombe, ambaye anachukua nafasi ya Charles Kichere aliyeteuliwa kuwa CAG, kabla ya uteuzi huo, Katarina alikuwa msajili mkuu wa mahakama ya Tanzania.

Wengine wanoapishwa ni Mhandisi Aisha Amour aliyeteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Kanali Francis Ronald Mbindi aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa kazi katika ofisi ya waziri Mkuu, kujaza nafasi iliyoachwa na Gabriel Pascal ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa naibu wakili wa Serikali .

Rais Magufuli amewaapisha majaji 12 wa Mahakama kuu ambao ni, Dkt. Zainabu Diwa Mango,  Edwin Elias Kakolaki, Dkt. Deo John Nangela,  Fredrick Kapela Manyanda,  Elizabeth Yoeza Mkwizu, Augustine Karichuba Rwizile, Ephery Sedekia, Angaza Mwaipopo, Joachim Charles Tiganga, Kassim Ngukali Robert, Said Mashaka Kalunde, Angela Antony Bahati.

Wengine wanaoapishwa ni viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti wa Tume, Mohamed Khamis Hamad Kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume, Fatma Rashid Khalfan kuwa Kamishina wa Tume, Thomas Paul Masanja kuwa Kamishna wa Tume, Amina Talib Ali kuwa Kamishna wa Tume, Khatibu Mwinyi Khatib Mwinyichande kuwa Kamishna wa Tume na Nyanda Josiah Shuli Kuwa Kamishna wa Tume.

LIVE IKULU: Rais Magufuli akiapisha viongozi mbalimbali
Manara ataja 'point' wanazotaka kwenye Ligi kuu

Comments

comments