Msanii wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha amesema kuwa mabinti wadogo wengi wao hawaolewi kwa sababu wanawaza starehe na hawafikirii kuhusu maisha zaidi ya starehe zisizo na tija.

Mbasha amesema kuwa kutokana na hali hiyo vijana wengi sasa wamekuwa wakioa wanawake wakubwa au ambao wamekomaa kiakili na wanaowaza maisha na si starehe.

“Vijana wa sasa wamefocus na maisha zaidi, hivyo wanahitaji mwanamke aliyekomaa ubongo ambaye wanaweza kufanya mipango ya maisha na kupaa kwa pamoja hadi kwenye ndoto zao. Hii ndiyo inapelekea wanawake wenye umri mkubwa kuolewa kwa kasi kubwa. Hivi vichenchede vinavyowazia kubandika kucha na kope bandia na kusingizia mahusiano ya uongo ili kupata Kiki na mimba hewa sasa havina soko vimebakia kuchuna viinua mgongo vya wanajeshi wastaafu,”amesema Mbasha 

Rais Lungu ang’aka, fedha alizotoa kununua wapinzani zatafunwa
UNESCO: Kuna upungufu mkubwa wa maji safi duniani