Baraza la mitihani la taifa leo tayari limeanika matokeo ya mtihani wa upimaji darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne.

Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema ufaulu katika mtihani wa upimaji wa darasa la nne umeongezeka kwa asilimia 26.21.

Katika mtihani wa upimaji kidato cha pili, wanafunzi 514,251 sawa na asilimia 90.04 kati ya wanafunzi 571,137 wamefanya vizuri katika mtihani huo na kuwawezesha kuingia kidato cha tatu.

Na kidato cha nne jumla ya watahiniwa 340,914 sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa 422,722 wamefaulu mitihani yao.

Tazama matokeo yao hapa chini.

MATOKEO KIDATO CHA NNE

MATOKEO KIDATO CHA PILI

MATOKEO DARASA LA NNE

Serikali yawataka mabalozi kuzingatia sheria, taratibu za nchi
Dkt Kayoka: Marekani kumuua Kamanda Soleimani ni kichekesho, walishirikiana naye (video)