Ndizi ni tunda lenye virutubisho vingi sana, ni tunda linalotumika kutengeneza vitu mbalimbali na ina kazi nyingi mwilimi ikiwemo, kuupa nguvu mwili, kupunguza mwili, kuulinda moyo, kuzuia viuvimbe katika figo, na kusaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.

Hata hivyo ulaji mwingi wa ndizi huashiria mwili kukosa virutubisho vya Protini na Fati kwenye mlo.

Japokuwa ndizi ni nzuri kiafya inasemekana kuwa ulaji wa ndizi kupita kiasi kunaweza kusababisha matatizo mengine ya kiafya kama yafuatayo

Kama ni mpenzi wa ndizi huu ni wakati sasa kutazama upande mwingine wa ndizi ili kujiepusha na mambo haya 5 yanaotokana na ulaji wa ndizi kupita kiasi.

 

  1. Kushindwa kupata choo (haja kubwa), ulaji wa ndizi zisizoiva kunaweza kusababisha upatikanaji wa choo kuwa mgumu au kutopata kabisa, kwani ndizi mbichi huwa na kiwango kikubwa cha stachi ambacho ni vugumu kwa mfumo cha chakula kumeng’enya aina hiyo ya chakula.
  2. Kusababisha uwiano mbovu wa virutubisho mwilini, kama ilivyo mwili unahitaji uwiano sawa wa virutubisho mwilini kwamba hakuna kirutubisho kinachotakiwa kuzidi au kupungua, endapo mtu atatumia ndizi kupita kiasi katika mlo wake utumbo unanafasi ndogo ya kuhifadhi aina nyingine ya chakula, kwa mujibu wa madaktari wa USDA binadamu kwa siku anahitaji ndizi mbili tu ili kuacha nafasi ya matunda mengine na vyakula vyenye virutubisho mwilini.
  3. Husababisha mtu kupata usingizi sana kwani ndizi ina asidi inayojulikana kama tryptophan ambayo hufanya mtu kupata usingizi mara kwa mara.
  4. Husababisha matatizo ya meno kutokana na kiwango cha sukari kilichopo kwenye ndizi.
  5. Huongeza unene wa mwili, endapo mtu akila ndizi kupita kiasi husababisha kuongeka kwa mwili kwani ndizi ina miliki kiasi kikubwa cha kalori mwilini, hivyo inashauriwa kwa siku mtu kutumia ndizi mbili tu.
  6. Husababisha maumivu ya tumbo ambayo yanatokana na gesi kujaa tumboni.

Video: Mkuchika awakingia kifua watumishi waliotumbuliwa na wakuu wa mkoa, wilaya
Muhimbili yathibitisha kumlaza Mbowe, aanguka ghafla