Kuna zaidi ya aina 100 za virusi wa Human papilloma huku aina 14 kati yake zikiwa na uwezo wa kusababisha aina mbalimbali za saratani mfano saratani ya koo, mlango wa kizazi na koromeo.

Mbali na saratani, Virusi vya Human papilloma vinaweza pia kusababisha athari zingine kwa afya ikiwemo masundosundo (warts) kwenye sehemu za siri na midomo.

Aidha Usambazwaji wake na kuambukizwa kwa mtu kunaweza kutokea kwa mtoto wakati mama anajifungua, pia kupitia aina mbalimbali za ngono (Uke, mdomo au sehemu ya haja kubwa). Kutokana na uwepo wa ngozi laini inayounda kinywa pamoja na sehemu ya nje ya midomo, watu wanaoshiriki ngono ya mdomo wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa virusi hawa ambao huleta shida ya masundosundo.

Dalili za ugonjwa huu zinaweza kuonekana baada ya wiki kadhaa, miezi au hata baada ya mwaka. Huu ni wakati ambao mhusika hataweza hata kukumbuka ni nani amesababisha yeye augue, hasa kama anao wapenzi wengi. Hii ni kwa jinsia zote.

credit@afyainfo

Rais Mwinyi asisitiza maboresho ya sheria kujenga uchumi wa buluu
Watano wa familia moja wauwawa Dodoma