Utamaduni wa kuweka wallet mfuko wa nyuma wa suruali kwa wanaume umekuwa ni jambo la kawaida lakini lenye madhara kiafya kupitia wataalamu wa afya wamesema kuwa tabia hiyo ya kuweka wallet mfuko wa nyuma unaharibu uwiano wa mwili katika kukaa, hui ‘twist’ mifupa ya nyonga.

Unapokalia wallet huweka mgandamizo mkubwa kwenye uti wa mgongo hivyo kuzifanya pingili zake zijisogeze kutoka kwenye mpangilio wake wa kawaida.

Wallets zinaweza pia kusababisha mgandamizo kwenye misuli ya Piriformis ambayo huathiri neva za sciatic (sciatic nerves).

Halikadhalika wallets husababisha matatizo makubwa ya uti wa mgongo pamoja na maumivu ya nyonga na mgongo kwa wanaume wengi pasipo kuelewa nini chanzo cha tatizo hili, matatizo haya yanaweza yasionekane moja kwa moja ndani ya muda mfupi lakini yakatokea muda mrefu baadae.

Wataalamu wa afya wanashauri kwa wanaume kuweka wallet kwenye mifuko ya mbele ya suruali,au kama unaamua kuiweka kwenye mifuko ya nyuma basi hakikisha hujaijaza vitu vingi sana kiasi cha kukufanya ukae kwa tabu.

Video: Mhalifu aliyetoroka Gerezani ''nilikalia mto ndoo''
Fursa ya Teknolojia kwa wanawake