Kufuatia mvua iliyonyesha alfajiri ya leo Januari 16, 2019 kwa takribani masaa matano maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam yameathirika na mvua hizo ambazo zimepelekea usafiri kuwa mgumu na baadhi ya barabara kufungwa.

Baadhi ya maeneo yameathirika pakubwa na mvua hizo kama vile Mwenge eneo la zahanati, lakini pia kulikuwa na ujenzi mkubwa wa utanuzi wa barabara ulikuwa unaendelea nao kwa kiasi kikubwa umeathiriwa na mvua hizo.

Pia eneo la Mwananyamala “Raound about” pamezingirwa na maji mengi yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Lakini pia barabara ya Jangwani ililazimika kufungwa kutokana na eneo hilo kujaa maji yaliyotokana na Mvua hizo.

Aidha, Mamlaka ya Hali ya Hewa imetabiri kuwa na vipindi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.

Dar: Abiria wa mwendokasi wabadilishiwa njia
Maporomoko ya theluji yaua 160

Comments

comments