Kanisa la mhubiri maarufu nchini Nigeria Temitope Balogun Joshua, maarufu TB Joshua limetangaza kuwa mhubiri huyo atazikwa karibu na makao makuu ya kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN mjini Lagos.

Mhubiri huyo aliyekuwa na umri wa miaka 57 alifariki Juni 5,2021 siku chache kabla ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

“Tunajiandaa kwa ibada ya kila wiki kukumbuka maisha ya Nabii TB Joshua.” taarifa ilisema.

TB Joshua, alizaliwa tarehe 12 mwezi Juni 1963 katika mji wa Arigidi huko Aoko kaskazini mashariki mwa jimbo la Kusini magharibi mwa Nigeria.

Hayati Tb Joshua, ndiye mwanzilishi wa kanisa la Sinagogi la mataifa yote SCOAN ambalo huhubiri moja kwa moja katika runinga ya Emmanuel TV mjini Lagos.

Samia aagiza viwanja vya mchezo kurekebishwa
Maandamano yatarajiwa mji mkongwe Jerusalem