Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya ​Chelsea na timu ya Taifa ya Ubelgiji Eden Hazard amesisitiza kuwa alikuwa upande wa mneja Jose Mourinho kabla ya hajatimuliwa kazi Stamford Bridge.

Katikati ya msimu wa  2015/16  Mourinho alitimuliwa kazi kwa mara ya pili katika klabu hiyo baada ya kushindwa kutetea taji la ligi kuu ya Uingereza walilolinyakua msimu uliopita.

Hazard ni miongoni mwa wachezaji walioshutumiwa kucheza chini ya kiwango ili kuhakikisha  Mourinho anafutwa kazi kutokana na mbinu .”Watu wanasema wanachojisikia, Ni kipindi ambacho sikuwa katika kiwango bora lakini sikutaka hata siku moja Mourinho  afutwe kazi,” Hazard aliliambia gazeti la   L’Equipe la nchini Ufaransa.

“Sikuwa na mwaka mzuri lazima niwe muwazi, ni upumbavu kusema nilihujumu timu kwa ajili ya kufutwa kazi kwa kocha,” alisema Hazard.

Tayari Mourinho amepewa kibarua cha kukinoa kikosi cha Manchester United msimu unaoanza mwezi Agosti.

Shomari Kapombe Ang'ara Zaidi Ya Wengine Azam FC
Simba Yaendelea Kuifumua Mtibwa Sugar