Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche amesema Shirika la Umeme nchini (TANESCO) halitafanikiwa milele kupata faida mpaka mwisho wa dunia.

Amesema kuwa shirika hilo limeingia mkataba usio na tija kwa taifa na kampuni ya uzalishaji umeme ya Songas ambapo amesema faida yote inachukuliwa na kampuni hiyo.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma, alipokuwa akichangia hoja katika mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati katika mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza kuwa kama mkataba huo utaendelea basi madeni ya TANESCO yatazidi kuongezeka maradufu.

“kamwe mpaka dunia hii inaisha TANESCO hawatapata faida kwasababu mkataba walioingia na Songas ni mkataba wa kihuni na wizi ndiyo unasababisha shirika hili kuendelea kuwa na madeni na hata dunia hii inaisha kama mkataba na Songas utaendelea kuwepo madeni ya TANESCO yataendelea kuwa makubwa,”amesema Heche

Aidha, ameongeza kuwa kitendo cha shirika hilo kuwa pekee linalozalisha umeme nchini bila ya kuwa na mshindani imechangia kwa kiasi kikubwa kuwa na mzigo wa kutoa huduma pamoja na madeni ambapo mpaka kufikia sasa linadaiwa zaidi ya bilioni 900.

Hata hivyo, hapo jana Bunge lilipitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ambapo jumla ya shilingi trilioni 1.69 imeizinishwa kwa matumizi ya miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida

 

 

Rushwa yazidi kuitafuna serikali ya Kenyatta
Magazeti ya Tanzania leo Mei 26, 2018