Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kusitisha zoezi la uwekaji alama au vigingi kwenye maeneo ya watu kwani zoezi hilo limejaa unyanyasaji.

Ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2018/19

Heche ameunga mkono ushauri wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Utalii na Mazingira iliyopendekeza usitishaji wa kuweka mipaka katika maeneo.

“Uwekaji wa vigingi katika ardhi na makazi ya watu usitishwe mara moja, sijui kama tunafikiri vizuri,wafugaji waiamua kuzuia hata siku kumi kuuza mifugo mnadhani tutapata wapi nyama,”amesema Heche.

Aidha, amesema kuwa wafugaji zaidi ya milioni 10 wanaishi Tanzania kama wakimbizi ambapo amesema kuwa serikali imekuwa ikiwatesa watu hao.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni wiki moja tu iliyopita huko Tarime Mkoani mara, mkuu wa wilaya na kundi lake walikwenda kwenye vijiji bila ya kutoa taarifa kwa viongozi husika.

 

 

Afya ya Jet Li yawa tete, ageuka mzee ghafla
Chukua tahadhari, aina tatu za uhalifu kwa simu za mkononi