Mbunge wa Tariime Vijijini, John Heche ameilaumu seriakli ya CCM kutumia fedha za wanachi kuwekeza katika mipango ya muda mfupi na kuishauri kuwa iwe inachukua mawazo yanayotolewa na wabunge mbalimbali pindi vikao vya bunge vinapoendelea

Heche amezungumza hayo leo bungeni pindi akichangia hoja juu ya taratibu ambazo zinazoendelea kuchukuliwa hivi karibuni za kuhamisha kituo cha mabasi ya mwendokasi ya UDART na kukihamishia Stendi ya mabasi ya mikoani Ubungo.

”Serikali hii inashauriwa mara nyingi, mimi nasikitika mipango ya seriakli ya CCM ni mipango ya miaka miwili miwili mwaka mmoja mmoja, ndio maana mipango mingi inafeli , na mngekuwa mnachukua mawazo hapa mnayafanyia kazi msingekuwa mnafeli” amesema Heche.

Kufuatia eneo ilipojengwa stendi ya mabasi ya mwendokasi jangwani ambako kumekumbwa na mafuriko makubwa mara baada ya mvua kunyesha mfulululizo jijini Dar es salaam na kusababisha ukuta wa Mto msimbazi kubomoka hali iliyopelekea maji ya mto huo kuvamia kituo cha mabasi ya mwendekosi, adha iliyosababisha idadii ya mabasi 29 kuharibika na kuhairisha safari zake huku baadhi ya wafanyakazi kupewa likizo mpaka jambo hilo litakapowekwa sawa.

Akiwa Bungeni Heche amesema Serikali imekuwa ikishauriwa mara nyingi na hajawahi kuwa sikivu katika mambo ambayo baadae yanakuwa ni janga kwa taifa kutokana na mipango yao mingi kuwa inafeli.

Amekumbushia wakati serikali ilipokuwa inapanga kujenga kituo cha mabasi ya mwendokasi Mnyika aliwahi kushauri serikali ya CCM juu ya eneo hilo la Jangwani kuwa linajaa maji.

Ameiomba Serikali ya CCM kuchukua mawazo bungeni na kuyafanyia kazi ili kuepuka upotevu wa pesa za wananchi na kuwa na mipango ya muda mrefu.

Mbowe: Hatuna hakika ni taratibu upi umetumika kufupisha kifungo chao
Serikali yazindua chanjo ya kudhibiti Ukimwi kwa 90%