Beki wa pembeni wa Arsenal  Hector Bellerin amesema hana shaka na mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez ambaye amekua akidhaniwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo katika kipindi hiki.

Dhana ya kuwa na tatizo la msongo wa mawazo, imeibuliwa na vyombo vya habari vya nchini England, kufuatia mpango wa mshambuliaji huyo wa kutaka kuhamia Man city kukwama siku ya mwisho ya dirisha la usajili mwishoni mwa mwezi uliopita.

Sanchez alicheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya AFC Bournemouth akitokea benchi, jambo ambalo liliendelea kuongeza hisia kwa mashabiki, kuhusu suala linalozungumzwa na kuandikwa kuhusu mshambuliaji huyo.

Bellerin amesema upande wake haamini kichozungumzwa kwa kipindi cha majuma mawili kumuhusu Sanchez, kutokana na kumfahamu vilivyo mshambuliaji huyo, ambaye amecheza nae kwa kipindi cha miaka mitatu sasa.

“Alexis yupo safi kwa asilimia 100, na hakuna lolote lenye ushahidi kuhusu msongo wa mawazo unaoelezwa na vyombo vya habari,” beki huyo aliiambia tovuti ya IBTimes.

“Hakupewa nafasi ya kuanza katika mchezo wa AFC Bournemouth baada ya kutokua na itimamu wa mwili, kutokana na kazi kubwa aliyoifanya akiwa na timu yake ya taifa, lakini ninakuhakikishia Sanchez yupo vizuri na ana malengo makubwa ya kuisaidia Arsenal katika mchezo ujao.”

Paul Pogba kuikosa Everton jumapili
Edinson Cavani avunja rekodi ya Ibrahimovic