Beki wa pembeni wa klabu ya Arsenal, Hector Bellerin atakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Hispania ambacho kitatatea ubingwa wa barani Ulaya, katika fainali za Euro 2016 zinazotarajiwa kuanza rasmi Juni 10 huko Ufaransa.

Bellerin, amepata nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi cha Hispania, baada ya kuthibitika kuumia kwa beki wa pembeni wa Real Madrid, Dani Carvajal ambaye kwa mara ya mwisho alionekana wakati wa mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid uliyochezwa mwishoni mwa juma lililopita mjini Milan nchini italia.

Mapema hii leo majibu ya vipimo vya Carvajal, vilimfikia kocha mkuu wa kikosi cha Hispania Vicente del Bosque, na imethibitika beki huyo aliyetolewa uwanjani huku akiwa anamwaga machozi kufuatia maumivu makali ya misuli ya paja, hatoweza kuwa fit kabla ya kuanza kwa fainali za Euro 2016.

Dani Carvajal akitolewa nje ya uwanja kwa usaidizi wa matabibu wa Real Madrid wakati wa mchezo wa fainali siku ya jumamosi.

Del Bosque, alizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliokuwepo katika kambi ya timu ya taifa ya Hispania na kuwaelezea habari hizo, lakini akaonyesha kuguswa na kitendo cha kumkosa beki huyo ambaye alikua muhimili mkubwa kwa Real Madrid, karibu msimu mzima wa 2015-16.

“Ninamtakia kila la kheri Carvajal katika kipindi hiki ambacho atakua akijiuguza, na sina budi kujiandaa na hatua ya kuziba nafasi yake kwa kumteua mchezaji atakaekua na vigezo vya kupambana wakati wote tutakapokua kwenye fainali za Euro 2116.” Alisema Del Bosque, ambaye anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Korea kusini utakaochezwa mjini Salzburg siku ya jumatano.

Juanfran

Kwa mantiki hiyo sasa kikosi cha Hispania kinasaliwa na mabeki wawili wanaocheza nafasi ya upande wa kulia ambao ni Juanfran (Atletico Madrid) pamoja na Bellerin (Arsenal).

Mkwasa Aishitukia Misri, Wanyama Na Kazimoto Watoa Neno
Jose Mourinho Aingiza Figisu Figisu Usajili Wa Mascherano

Comments

comments