Mbunge wa Buhigwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Albert Obama, amemjibu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango juu ya adhima yake aliyotangaza jana kutaka ubunge kwenye jimbo hilo uchaguzi mkuu ujao 2020, kwa kusema hana wasiwasi.

Obama ametoa jibu hilo leo, Juni 12, Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hoja kwenye bajeti kuu ya Serikali na kubainisha kuwa yeye ni mashine wa Buhigwe hivyo kwenye uchaguzi mkuu CCM watampitisha tena agombee.

“Ukija kwenye orodha ya majina yangu hapa Bungeni utaambiwa Obama anaitwa nani, utaambiwa ni mashine ya jimbo, mashine ya kusaga na kukoboa…., Buhigwe wanajua tulikotoka, tuliko, na tunakoelekea niseme 2020 Magufuli hapa, Obama hapa” Amesisitiza Mbunge huyo.

Hayo yamejiri baada ya jana, Waziri Mpango ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa, wakati akihitimisha kusoma Bajeti ya Serikali kutoa wito kwa wananchi wa Buhigwe kumchagua awawakilishe Bungeni.

Hata hivyo Mbunge Obama hajasita kutoa pongezi kwa Waziri Mpango kufuatia dua yake ya kuwaombea wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti kupita bila kupingwa kwani yeye ni mmoja wapo.

Makaburi ya watu wengi yagunduliwa Libya
Ushahidi: Waziri Mkuu msaafu alivyolipa majambazi kumuua mkewe kisa mchepuko