Helikopta ya mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, Vichai Srivaddhanaprabha jana iliteketea kwa moto baada ya kulipuka na kuungua nje ya Uwanja wa King Power jijini Leicester.

Tukio hilo lilitokea dakika chache tu baada ya Leicester City kulazimishwa sare ya kufungana bao na 1-1 West Ham, ambapo wageni wakitangulia kwa bao la Fabian Balbuena dakika ya 30 kabla ya Wilfred Ndidi kuwasawazishia wenyeji, dakika ya 89.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema kwamba waliona helikopta hiyo inaungua muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanjani hapo.

Aidha, chanzo cha kulipuka kwa helikopta hiyo inaelezwa kuwa ni hitilafu za kwenye injini lakini mashabiki walishitushwa na tukio hilo na wengine walibubujikwa na  machozi baada ya ndege hiyo kuingizwa ndani ya Uwanja kwenye eneo la kuegeshea magari.

Vilevile haijulikani akina nani walikuwepo kwenye chombo hicho wakati kinateketea kwa moto, lakini mmiliki wa Leicester mwenyewe alikuwa anaangalia mechi.

Srivaddhanaprabha alikuwa mchora ramani wa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England walilochukua Leicester katika msimu ambao walipanda kutoka daraja la Kwanza, mwaka 2016.

Video: Maalim Seif aweka msimamo wa kuhamia Chadema, kustaafu, Saa zahesabika waliotafuna mali CCM
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 28, 2018