Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB) na Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wameingia makubaliano ya kutoa mkopo wa asilimia 100 kwa wanafunzi wanaotoka kaya maskini nchini.

Aidha, bodi imetenga Sh. billion 570, kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi 160,000 kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Akizugumza na waandishi wa habari jana wakati wa kusaini makubaliano hayo katibu mkuu Ikulu ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Moses Kusiluka, alisema serikali inadhamira kubwa ya kuhakikisha wanafunzi wote wanapata mikopo kwa asilimia zote ili waweze kutumiza ndoto zao.

Alisema lengo lao ni kuona mikopo inapatikana kwa walengwa halisi ili kuondoa mkanganyiko watu kupata ambao sio kutoka kaya maskini.

”Serikali ina hakikisha dhamira ya watanzania wahitaji wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu wanapata mikopo na kupata elimu ya juu”amesema Kusiluka

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 17, 2021
Tatizo la mafuta sasa basi - Majaliwa