Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga amesema Watendaji wa kituo hicho wanapewa vitisho kutokana na kazi wanazofanya

Amesema hayo mbele ya Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora waliokuwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu Mathew Mwaimu walipotembelea ofisi za LHRC Jijini Dodoma

“Hata rangi tunayotumia wanaifananisha na chama fulani cha upinzani, sisi hatufungamani na upande wowote kinachotuponza ni kutetea demokrasi tu.”amesema Henga

Kwa mujibu wa Henga amesema pamoja na kazi nzuri zinazofanywa na watumishi wake, kinachowaponza ni kutafuta demokrasia kwani wamekuwa wakipishana na Serikali wakidaiwa kuwa wanaviunga mkono vyama vya upinzani

Aidha ameeleza wanavyonyimwa taarifa na haki ya kufuatilia baadhi ya mambo ikiwemo ombi la kufuatilia uchaguzi wa serikali za mitaa 2019

 

Mgonjwa wa Corona agundulika New Zealand
Balozi kijazi ateuliwa tena