Klabu ya Manchester United, inakaribia kumsajili kiungo kutoka nchini  Armenia na klabu ya Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan kufuatia mazungumzo baina ya pande hizo mbili kwenda sawa bin sawia.

Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini Engalnd, Man Utd wanapewa nafasi kubwa ya kukamilisha usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, baada ya kukubali kutoa ada ya uhamisho ya Pauni milioni 26.3.

Mkhitaryan amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia klabu ya Dortmund, na ameonyesha kuwa tayari kuihama klabu hiyo na kutimkia katika ligi ya nchini England huku akihitaji kuwa chini ya Jose Mourinho.

Kiungo huyo ambaye husaidia kupeleka mashambulizi kwa timu pinzani, amekua muhimili mkubwa katika kikosi cha Dortmund tangu mwaka 2013 aliposajiliwa akitokea nchini Ukraine alipokua akiitumikia klabu ya Shakhtar Donetsk, ambayo ilimuachia kwa ada ya usajili ya Pauni milioni 23.5.

Msimu uliopita alifanikiwa kufunga mabao 18 na kutoa pasi zilizozaa magolo 25 katika michuano yote aliyocheza na mwishoni mwa msimu huo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi ya Bundesliga.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Armenia, Mkhitaryan amecheza michezo 59 na kufunga mabao 19.

Papa Francis: Kanisa Halina Mamlaka ya Kuhukumu
Lionel Messi Atangaza Kustaafu Soka