Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amekanusha taarifa zilizozagaa kuwa alimshawishi Alexis Sanchez kuhamia katika Klabu ya Manchester United.

Sanchez, alijiunga na Manchester United Jumatatu kwa makubaliano ya kubadilishana wachezaji ambapo Henrikh Mkhitaryan alihamia Arsenal, amesema kuwa alikuwa amezungumza na nyota huyo wa zamani.

“Nakumbuka mazungumzo niliyozungumza na Henry, ambaye alibadilisha Klabu kwa sababu sawa na zangu, sasa ni zamu yangu,”amesema Sanchez

Aidha, kijibu shutuma dhidi yake, Henry amesema kuwa hakuwa na taarifa yeyote kuhusu kuhama kwa Sanchez kwenda Manchester United mpaka alipoona taarifa kwenye vyombo vya habari.

Sanchez mwenye umri wa miaka, 29, amesaini mkataba wa miaka minne na nusu na atakuwa analipwa Euro 14m kwa mwaka.

 

Wafanyiwa upasuaji wa moyo bila kufungua kifua
Karia atuma salamu za rambirambi msiba wa Ntambi, Ismail Suma