Staa wa filamu, mtunisha misuli na mwanasiasa, ambaye amewahi kuwa Gavana wa Jimbo la Califonia nchini Marekani, Arnold Schwarzenegger leo anasherekea siku yake ya kuzaliwa na anatimiza miaka 7o.

Anold amezaliwa siku kama ya leo mwaka 1947, huko Thal, Austria, mwaka 1986 Aprili 26, Anold alimuoa Maria Shriver na mwaka 2011, waliachana na kupeana talaka huku wakiwa na watoto wanne,  Katherine, Christina, Patrick na Christopher.

Staa huyo kwa mara ya kwanza amepata kufahamika kwa watoto na watu wazima kupitia filamu ya ‘The Terminator’.

Anold Schwarzenegger amekuwa Gavana wa jimbo la Califonia kwa takribani miaka nane, ameongoza kuanzia mwaka 2003 hadi 2011, na kupokelewa na Gavana Edmund G, ‘Jerry Brown’.

Kupitia mazoezi ya kunyanyua vyuma vyenye uzito na utunishaji Misuli Schwarzenegger akiwa na miaka 20 ameingia katika orodha ya kuwa mmoja kati ya kijana mdogo kushinda Mr. Universum kwa takriban mara saba.

Katika siku yake hii muhimu miongoni mwa mmarafiki na mastaa wenzake walioonekana kumtakia maisha marefu na yenye Baraka tele. Muigizaji Sylvester Stallone kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika

”Pre – HAPPY BIRTHDAY ARNOLD!!!! As long as you live and beyond, you’re always going to be the “BIG MAN ” Who set the bar so high that it will never be surpassed , an action hero legend!”.

 

 

Majaliwa: Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji nchini
Video: Naibu Waziri wa elimu aagiza walemavu wajengewe vyoo vyao