Ander Herrera anasema kuwa anapata faida kubwa kutoka na uzoefu wa kushindania nafasi ya kucheza na wachezaji wazoefu na wakubwa kama Bastian Schweinsteiger na Michael Carrick katika kiungo cha Manchester United lakini anawaonya wakubwa zake hao kuwa atafanya kila analoweza kuhakikisha yeye anakuwa chaguo la kwanza katika nafasi hiyo.

Mhispania huyo anaamini kuwa ushindanio katika kiungi cha klabu yake umeongezeka na umekuwa ni wenye afya baada ya kusajili kwa Schneiderlin wakati wa uhamisho wa kiangazi. Herrera aling’ara sana katika mchezo wa ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Everton Jumamosi ambapo alifunga goli la pili na kutoa pasi ya mwisho ya goli kwa Wayne Roonery aliyefunga goli la tatu baada ya Schneiderlin kufungua kitabu cha magoli katika mchezo huo.

Baada ya kuwa katika kipindi cha kuingia na kutoka katika kikosi cha kwanza chini ya Louis van Gaal, Herrera sasa anataka kukabidhiwa nafasi hiyo katika kikosi cha kwanza na akiamini kuendelea kuchezaji wa wazoefu hao kikosini kunazidi kumjenga.

“unachukua faida hiyo kutoka kwa wazoefu wa sehemu ya kiungo. unapocheza na wachezaji wazuri unapata faida” Herrera ameuambia mtandao wa klabu yake ‘manutd.com.

 

Ronald Koeman Kubaki St Marries
Vumbi La Ligi Kuu Kutimka Tena Kesho