Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Hersi Said amesema Klabu hiyo inapaswa kuendeshwa kwa kufuata misingi ya ushirkiano na Taasisi nyingine za Michezo ndani na nje ya nchi.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo, huku kukiwa na tetesi za mara kwa mara zikieleza klabu ya Young Africans imekua haina mahusiano mazuri na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.

Hersi amesema Soka kwa sasa limepanuaka na linaakisi ushirikiano ama uhusiano baina ya Taasisi na Taasisi, na kama kuna tofauti zozote, atahakikisha anazimaliza kwa kukaa chini na wahusika, na kuifanya Young Africans kuwa imara.

“Hauwezi kuwa na uongozi ambao unaendesha mpira bila kuwa na mahusiano mazuri, mpira wa sasa hivi una mikono mikubwa sana, kuna wenzetu kutoka klabu mbalimbali tunapaswa kushirikiana nao, kuna wenzetu wa TFF tunatakiwa kushirikiana nao, kuna bodi ya ligi, kuna baraza la michezo kuna wizara ambayo ndio serikali, azma yangu ni kuhakikisha Young Africans inajenga mahusiano mazuri na taasisi zote hizi na zingine”

“Unaweza kuona jinsi tulivyo na mahusiano mazuri na jamii, klabu hii imekuwa karibu kila mchezo tunatoa ushirikiano na jamii mbalimbali kwa misaada kwa wenye uhitaji na mambo mengine, changamoto hazikosekani nikiri zipo, rapsha zinaweza kuwepo kidogo kwa kuwa hii ni klabu ya watu wengi kwa kuwa kila mtu ana mtazamo wake”

“Sisi kama viongozi tunapaswa kulibeba hili jambo kwenye uhalisia wake na kutafuta suluhisho, haliwezi kupatikana kama watu mtashindwa kukaa na kuweka mambo sawa, niseme tu kwangu mimi suala la mahusiano ni muhimu sana siwezi kuendesha hii klabu peke yangu, lazima tuwe na mahusiano yenye afya na taasisi zingine na hii ndio hatua ambayo itatufanya tuwe na mafanikio” amesema Hersi

Jupiter kukatiza jirani na uso wa Dunia baada ya miongo sita
Kocha Mgunda: Primeiro de Agosto wanatumia nguvu, akili nyingi