Rais wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans, Hersi Said amekiri kwa mara ya kwanza kuwa na mzigo mkubwa wa kuiendesha klabu hiyo, yenye historia pana ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Hersi alichaguliwa kuwa Rais wa Young Africans miezi miwili iliyopita, akigombe nafasi hiyo pekee yake, huku Wanachama na Mashabiki wengi wakiamini mafanikio chini ya utawala wake.

Kiongozi huyo amesema gharama za kuendesha Klabu hiyo ni kubwa sana lakini Uongozi wake unapambana kutafuta fedha kuhakikisha klabu inajiendesha yenyewe.

“Katika klabu kubwa kama Young Africans kuna maeneo mengi ambayo yanaongeza gharama za uendashaji wa klabu, mfano mwanzo mwa msimu unatakiwa ufanye usajili, ili ufanye usajili uliobora unatakiwa uwe na bilioni moja mpaka bilioni moja na nusu mezani”

“Chukulia mfano kama msimu uliopita tulipokwenda kucheza na Geita Gold na baadae Simba SC, ilihitajika tuwe na milioni 100, kwa ajili ya chakula, hoteli na usafiri wa ndege kwenda na kurudi na usafiri mkiwa ndani ya mkoa” amesema Hersi

Wakati wa Kampeni za kuwania kiti cha Urais Hersi Said aliahidi kuifanya Young Africans kuwa klabu itakayojiendesha yenyewe na kuacha mfumo tegemezi, ambao umekua ukitumika kwa miaka nenda rudi.

Mtanzania kutumia betri chakavu kuzalisha umeme
Afisa habari KMC FC aishangaa Simba SC