Meneja mpya wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amewaachia mtihani viongozi wa klabu hiyo kwa kutaka kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ghana na klabu bingwa nchini Italia Juventus, Kwadwo Asamoah asajiliwe huko Stamford Bridge.

Asamoah ni sehemu ya wachezaji walioorodheshwa na meneja huyo, kwa ajili ya kutimiza mikakati ya kukisuka upya kikosi cha Chelsea, ambacho msimu uliopita hakikufanya vyema kwenye ligi ya nchini England.

Conte ambaye kwa sasa ana jukumu la kukinoa kikosi cha Italia kwa ajili ya fainali za Euro 2016, ameagiza mchakato huo kufanywa huku akiamini hakuna kitakacho shindikana kufuatia kiu ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic, ya kutaka kuona The Blues inarejea katika hali yake ya ushindani.

Tayari uongozi wa Juventus umeshatangaza thamani ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, kwa kusisitiza kufanya biashara kwa kupokea kiasi cha Euro milioni 20-25 kama ada ya uhamisho.

Nabil Fekir Kumfuata Dimitri Payet West Ham Utd
Sugu hatarini, adaiwa kuwatusi wabunge wa CCM