Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu HESLB imetangaza orodha ya wanafunzi 47,305 watakaopata mikopo ya awamu ya kwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 11, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema kati ya wanafunzi 47,305 wanawake ni 20,341 sawa na asilimia 42.63 na wanaume ni 26,964 sawa na sawa na asilimi 57.

Badru amesema kuwa tayari fedha zimeanza kupelekwa vyuo mbalimbali na kuwataka wanafunzi kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mikopo, maarufu SIPA na kujiandaa kwenda chuo kujisajili.

Aidha bodi hiyo inatarajia kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 150.03, kutoa mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Pompeo apuuzia matokeo ya Uchaguzi wa Rais
Rais Magufuli kuhutubia Bunge kwa mara ya kwanza