Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, HESLB imetangaza mfumo mpya wa kielektoniki wa ulipaji madeni ya waliokuwa wanufaika wa mikopo, ambapo mfumo huo utajulikana kwa jina la ‘Goverment Electronic Payment Getway’ (GEGP).

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Nchini, Abdulrazack Badru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mfumo huo utarahisisha uwazi wa kwenye ukusanyaji wa fedha hizo na utamfanya mdaiwa kulipa mahali popote alipo pamoja na kutoa fursa ya kuongezeka kwa mapato ya bodi hiyo.

“Tumekamilisha utaratibu wa mfumo wa serikali wa kukusanya mapato (GEPG), mwajiri na wanufaika watatakiwa kujiunga kwenye mfumo huu mpya wa GEPG ili kulipa madeni wanayodaiwa na serikali,” amesema Badru

Aidha amesema kuwa waajiri ambao watashindwa kulipa madeni ya wafanyakazi ambao walikuwa ni wanufaika, wataanzishiwa operesheni maalumu ya kupitia maofisini kwao ili kuwabaini wasiolipa mikopo ya bodi.

Kwa upande wake, mtaalamu wa GEPG, Baziri Bajunia  amesema kuwa mfumo huo umekuwa ukitumika sasa hivi na taasisi nyingi ambazo zinafanya malipo kwa taasisi za serikali, ni utaratibu ambao hata taasisi nyingine za kifedha zinautumia.

Masauni atoa onyo 'Msithubutu kuwaazimisha silaha wahalifu'
Kisa cha Mbowe kuporwa ofisi yake ya ubunge