Na Martin Nyoni; Zanzibar 

Zikiwa zimebaki saa kadhaa kabla ya kuanza kufanyika kwa uchaguzi wa marejeo visiwani Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametoa taarifa yake ya mwisho kabla ya kuanza kwa zoezi hilo.

Akiongea na waandishi wa habari leo visiwani humo, Jecha amesema kuwa tayari vifaa vyote vya kupigia krua vimesambazwa kwenye vituo vyote vya kupigia kura vya Pemba na Unguja.

Jecha amesema kuwa maandalizi yamekamilika kwa kiwango cha kuridhisha na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo bila hofu.

Aidha ameongeza kuwa vitu vitafunguliwa majira ya saa moja za asubuhi na kufungwa majira ya saa kumi za jioni, hivyo Kuwataka wapiga kura kujitokeza mapema Katika vituo vya kupigia kura.

Hii ni taarifa ya mwisho ya Jecha kabla ya kuanza zoezi la kupiga kura, taarifa zake zitakazofuata zitakuwa zikizungumzia uchaguzi wa marudio utakaokuwa umeshafanyika.

Uchaguzi huo unavuta hisia za wafuatiliji wa masuala ya siasa kutokana na kuwepo kwa msuguano mkali baina ya chama tawala (CCM) ambacho kimekuwa kikipigia chapuo kurejewa kwa uchaguzi huo, na Chama kikuu cha upinzani visiwani humo (CUF) ambacho kinaupinga kwa madai kuwa uchaguzi tayari ulishafanyika Oktoba 25 na kinaamini kuwa mgombea wake wa urais, Maalim Seif Sharif Hamad alishinda.

Uchaguzi huo wa marejeo hapa vicwani humo unafanyika huku kukiwa na ulinzi mkali wa jeshi la wananchi wa Tanzania ambao wameimarisha ulinzi na usalama mahususi kwa shughuli za serikali, Pemba na Unguja.

Maeneo ambayo yamukuwa na ulinzi mkali ni pamoja na bandari ya Zanzibar, Ofisi za ZEC pamoja na Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC).

 

TCRA yawalinda Mke wa Rais Magufuli na Bi. Samia Suluhu Mtandaoni
Rais Magufuli ateua wakurugenzi wakuu wapya NSSF, TBC na RAHCO