Uongozi wa Clouds Media Group hatimaye umetangaza tena tarehe na mahali patakapo fanyika tamasha la Fiesta mara baada ya kuhamishwa kutoka katika viwanja vya Leaders Jiji Dar es salaam na kupelekwa Tanganyika Pekas.

Tamasha hilo ambalo lilikuwa lifanyike 24/11 mwaka huu na kuahirishwa kutokanan na barua iliyotolewana uongozi wa wilaya ya Kinondoni kulitaka tamasha hilo lifanyike katika viwanja vya Tanganyika Pekas Kawe, kwa madai kwamba eneo amabalo tamasha hilo lingefanyika lingeleta taharuki kutokana na kelele zitakazo jitokeza.

Tamasha la Fiesta ambalo lilikuwa limeshafanyika takribani mikoa 15 ya Tanzania, ambapo lilikuwa linafanya kilele cha tamasha hilo hapa Jijini Dar es saalam na kuahirishwa, Clouds Media imetangaza kufanyika kwa tamasha hilo tarehe 22 desemba mwaka huu ambapo tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Posta Jiji Dar es salaam.

 

 

Ofisa Elimu azuia Wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika kwenda likizo
Video: Sababu Mwalimu Nyerere kuitwa 'Baba wa Taifa'