Gazeti la ‘France Footbal’ limetoa orodha ya wachezaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha pesa kwa mwaka mzima kupitia mishahara pamoja na matangazo ya biashara wanayoyafanya na baadhi ya makampuini makubwa duniani.
Pesa hizo kwa mwaka pia zimejumuisha ongezeko la malipo (Bonus) ambayo wanayapata kupitia mikataba waliyosaini dhidi ya viongozi wa klabu wanazozitumikia kufuatia mafanikio wanayopata kwa kuwa sehemu ya kutwaa mataji ama kufikia lengo lililokusudiwa.
1. Lionel Messi, euros milioni 74

2. Cristiano Ronaldo, euros milioni 67.4

3 Neymar da Silva Santos Júnior, euros milioni 43.5

4. Zlatan Ibrahimovic, euros milioni 28.5

5. Thiago Silva, euros milioni 26.5
6. Angel Di Maria, euros milioni 26
7. Gareth Bale, euros milioni 24.5

8. Thomas Müller, euros milioni 23.6

9. Wayne Rooney, euros milioni 22

10. Andrés Iniesta, euros milioni 21.5