Ligi kuu ya Uingereza inaendelea leo ambapo mechi kubwa ni ile itakayopigwa katika dimba la Anfield wakati majogoo wa Liverpool wakiwakaribisha Manchester United.

Machester United watakuwa na mshambuliaji wao Romelu Lukaku ambaye siku za usoni anaonekana kujenga urafiki na nyavu akiwa amefunga mabao 7 katika mchezo 7 ya ligi kuu.

Pamoja na ukali wake wote wa kufunga mabao, historia inaonyesha kuwa Romelu Lukaku huwa anapata wakati mgumu sana mbele ya Liverpool ambapo katika michezo 7 aliyocheza dhidi ya Liverpool amefanikiwa kufunga bao moja tu.

Kama Lukaku atafunga bao katika mchezo wa leo atakuwa mchezaji wa kwanza Epl kufunga mfululizo katika mechi 8 za mwanzo.

Manchester United watawakosa Paul Pogba na Maroane Fellaini huku Liverpool wakimkosa mshambuliaji wao raia wa Senegal Sadio Mane aliyepata majeraha ya misuli ya paja akiwa anaitumika timu yake ya taifa.

 

Mama wa mgombea urais Rwanda adai kunyanyaswa
Video: Prof. Mwandosya atema nyongo, Sharti la uchaguzi lazua hofu CCM