Kwa mujibu wa kampuni ya Pantone ambayo inajulika duniani kwa kuteua rangi ambayo itatawala kwa mwaka mzima, rangi ya mwaka 2020 ni classic blue.

Classic blue ni rangi ya bluu au samawati ya kale ambayo ni nzito kudogo kulinganisha na bluu bahari.

Imeelezwa kuwa kupitishwa kwa rangi hii hakuhusishi nguo pekee, bali ubunifu wa mitindo mbalimbali kama viatu, mkoba, matangazo hata hereni na mikufu.

Kwamujibu wa mtandao wa ADpro umeeleza kuwa rangi hiyo imeteuliwa na Pantone ambayo ilianza kazi hiyo mika 20 iliyopita.

“Tunapoiangalia dunia ilivyotuzunguka, tunajua tunaishi na vitu vingi ambavyo havipo sawa kiasi kwamba wakati mwingine tunaona hatupo salama” amefunguka Leartice Eiseman ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya rangi iliyo chini ya pantoone.

Na kuongeza kuwa ” Bluu, kwa kuangalia hisia na saikolojia, imekuwa ikiwasilisha kiwango fulani cha utulivu na kutegemeana. ni rangi ambayo unaweza kuitegemea”

Tanzania, India kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia, kukuza maendeleo
Maziwa mtindi kinga dhidi ya mafua

Comments

comments