Vijiwe vingi vya Bodaboda vimekua na utaratibu wa kubeba abiria kwa foleni maalum, kijiwe cha bodaboda cha Kawe Jijini Dare es Salaa na wao wanautaratibu wa kubeba abiria kwa foleni, lakini wao wameenda mbele zaidi na kuchonga namba ambayo kila mmoja anapewa na kujua yeye ni namba gani kubeba abiria .

Aidha inasemekana mfumo huo katika kijiwe hicho umesaidia kutatua baadhi ya changamoto za vijiweni ikiwemo kupungua kwa ajali za kizembe kwa kumkimbilia mteja.

Wakizungumza na Dar24 Media madereva bodaboda hao wamesema kuwa mfumo huo kwao umekuwa na manufaa makubwa ikiwemo kusaidia boda boda wote kuingiza kipato kwa kuafuata utaratibu.

Hali kadhalika faida nyingine wanayoipata kupitia mfumo huo ni kumjengea mteja kujiamini ambapo wamebainisha kuwa endapo bodaboda akifanya uhalifu ni rahisi kumpata na kumchukulia hatua.


Nabi aitangazia njaa Ihefu FC
Gomes aupa tano uongozi Simba SC