Mshambuliaji wa Bercelona Lionel Messi ameweka wazi kuwa anaweza kujiunga na klabu ya Newell’s Old Boys inayoshiriki ligi kuu nchini Argentina pindi atakapo ondoka Barcelona.

Messi amesema kuwa angependa kumalizia soka lake katika klabu hiyo iliyomuibua tangu akiwa na miaka sita kabla ya kujiunga na Bacerlona mwaka 2001 akiwa na miaka kumi na mbili.

Staa huyo anayetarajia kuiongoza timu ya taifa ya Argentina kwenye fainali za kombe la dunia nchini Urusi, amefunguka kuwa Barcelona itakuwa timu pekee atakayochezea barani ulaya.

. “Mara zote nimekuwa nikisema nataka kucheza soka la Argentina, sina uhakika kama itatokea lakini nimekuwa nikifikiria’ Messi amekiambia kituo cha runinga cha El Trece cha nchini Argentina.

“itakuwa ni Newell’s, hakuna sehemu nyingine, ningependa kufanya hivyo walau kwa miezi sita, huwezi jua nini kitatokea’’ ameongeza Messi.

Lionel Messi anatarajia kuingoza Argentina kwa mafanikio kwenye fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwezi juni mwaka huu kufuatia timu hiyo kufanya vizuri kwenye michezo ya hivi karibuni, Mara ya mwisho Argentina kushinda kombe la dunia ilikuwa ni mwaka 1986 wakati ikiongozwa na Diego Maladona.

Lampard ala shavu Derby County
'Kwa Ngwaru' ya Harmonize yaweka rekodi Afrika Mashariki