Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa anatamani angekuwa Waziri wa Michezo ili ahakikishe timu zote za Tanzania zinazoshiriki mashindano hayo zinafanya vizuri.

Ameyasema hayo jijini Mbeya wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi jijini humo iliyolenga kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Rais Magufuli amesema kuwa, ameambiwa Kyela kuna tatizo la umeme, kwamba umeme unakatikatika halafu kukatika kunaumiza sana, huku unakuta unaangalia mpira umeme unakatika halafu goli ndiyo lilikuwa linaingia.

”Waziri wa Michezo anatoka Kyela ingawaje kwenye timu ya vijana ameniangusha, yaani mpira uchezwe kwenye uwanja wako timu yako halafu mnatandikwa hapohapo yaani ajabu kweli, Vitu ambavyo vinaniboa ni kufungwa kwa timu zangu, huwa najisikia hovyo, natamani siku moja niwe Waziri wa Michezo halafu waone mimi nitakavyokuwa, timu nitaipanga mwenyewe,” ameongeza Rais Magufuli.

Aidha kuhusiana na Waziri wa Habari, Utamaduni sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Rais Magufuli amesema kuwa huenda watu wengi wa Kyela wakawa hawamfahamu kiongozi huyo.

“Mwakyembe alikuwa Naibu Waziri wangu alinisumbua sana, amewahi kunyweshwa sumu akapelekwa nje kwa sababu ya kusimamia haki, inawezekana nyinyi hamumjui Mwakyembe.” amesema Rais Magufuli

Watendaji wanaoficha mapato kuhamishwa bila malipo Njombe
Kiongozi wa IS aliyedaiwa kuuawa ajitokeza kwenye video na ujumbe