Donald Trump amewaamuru maafisa wake wa upelelezi kutofuatilia uchunguzi mpya kuhusu kashfa ya barua pepe iliyomkabili mpinzani wake Hilarry Clinton.

Donald Trump alifafanua na kusema kwa kufanya hivyo inaweza kuzua migawanyiko zaidi. Ufafanuzi huo ulikuja baada ya wafuasi waTrump kulalamika na kumtaka Clinton afungwe kama Rais Trump alivyoahidi hapo mwanzo. Kutokana na ufafanuzi huo baadhi ya wafuasi walimnukuu Trump kama msaliti.

FBI walimuondolea Clinton makosa lakini wafuasi wa Trump walikuwa wakiimba ‘Lock her up’ (mfunge jela)

Mchunguzi wa masuala ya kisiasa Ann Coulter, ambaye ni mhafidhina, aliandika kwenye Twitter “ Whoa! Nilidhani tulimchagua @realDonald Trump kuwa Rais. Tulimfanya FBI,& DOJ? Kazi yake ni kuwateua kufanya kazi yao”

Kisha alifuatiliza na ujumbe  mwingine ;hakuna rais anayefaa kuwa akiwazuia wachunguzi kufanya kazi yao. #EqualUnderLaw (Wote sawa mbele ya sheria)

Maadhimisho ya kupinga ukatili wa kijinsia kuanza Novemba 25
Bob Bradley: Donald Trump Ataivurugia Marekani