Wachezaji Abdul Hillary, Hassan Kabunda wamejiunga na wenzao katika maandalizi ya mchezo wa Mzunguuko wa 18 Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City FCambao watakua wenyeji wa KMC FC juma hili.

Wawili hao hawakuwa kikosini kwasiku kadhaa kufuatia kuwa majeruhi, huku taarifa za madaktari wa timu hiyo zinaeleza wamepona na wapo tayari kupambana.

Hassan Kabunda aliumia katika mchezo dhidi ya Simba SC na hivyo kushindwa kucheza katika michezo miwili ambayo ni dhidi ya Ihefu pamoja na JKT Tanzania.

Mchezaji mwingine ambaye ameungana na wenzake katika mazoezi ya leo ni pamoja na David Brayson ambaye alikuwa kwenye Timu ya Taifa ya Vijana Ngorongoro Herous.

Hata hivyo hadi sasa wachezaji wengine ambao hawajaweza kurejea mazoezini ni pamoja na Kenny Ally, Andrew Vicent (Dante) pamoja na golikipa Rahim Sheih ambapo wote wanasumbuliwa na majeraha.

Dante alipata majeraha katika mchezo dhidi ya SimbaSC na hivyo kucheza kwa muda mfupi katika mchezo dhidi ya Ihefu na hivyo kushindwa kuendelea katika mchezo mwingine dhidi ya JKT Tanzania.

KMC FC itacheza dhidi ya Mbeya City FC katika uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya January 02, 2021 na kwamba kikosi hicho kinajiandaa kuhakikisha kwamba kinafanya vizuri katika mchezo ambapo katika mzunguko wa kwanza waliweza kuibuka na ushindi wa magoli manne kwa sifuri.

Wananchi Nzega watoa kongole kwa Airtel
Mngereza kuzikwa Jumatano Same