Kiungo mkabaji wa Azam, Himid Mao amesema pambano lao dhidi ya Simba lilikuwa gumu kinyume na matarajio yao.

Timu hizo zilikutana juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara, ambapo zilitoka suluhu ya mabao 2-2 matokeo ambayo yameendelea kuwabakiza Azam kileleni.

“Mchezo ulikua mgumu tofauti na tulivyotarajia. Kama ulivyoona simba walicheza na viungo sita na sisi tulicheza watatu, na mfumo wao pia ndio ilikua tatizo kama unavyojua mfumo wa 4-4-2 aina ya almasi unajaza watu wengi katikati, hapo ndipo tatizo kubwa lilipokua na hata ukiangalia washambuliaji wao ni viungo kiasili sio washambuliaji asilimia zote.

Katika mahojiano hayo na mtandao wa dar24, Himid pia alizungumzia uchezaji wao kiujumla na kusema ulikuwa chini ya kiwango chao cha kawaida.

“Utendaji wa timu haukuwa mzuri kiukweli, karibia nusu ya wachezaji wetu hawakuwa katika viwango vyao vya kawaida”

“Kikwazo ni mechi ya kwanza baada ya Mechi za kitaifa, hata kocha huwa ana hofu sana na mechi zinazokua baada ya wiki ya kimataifa kwakua wachezaji wengi wa Azam wanacheza timu tofaut za taifa. Kwahiyo tunaporudi tunakua kama mnaanza upya hata kasi yetu tuliyomalizia mechi mbili kabla ya Mechi Za kitaifa imekata.”

Akiongelea kuhusu swala ya yeye kuhitaji kupumzishwa baada ya kucheza Mechi nyingi Za kitaifa Na Klabu Kwa mfululizo:

“Mwalimu aliniambia hivyo baada ya kipindi cha kwanza kuwa naonekana nimechoka na sina nguvu yangu ya kawaida, ananifahamu vizuri akinipa mapumziko pia ni jambo jema kwakuwa nimecheza mechi nyingi sana zenye ushindani ndani ya muda mfupi “

Akiongelea kuhusu kiwango wake kwenye Mechi dhidi ya simba:

“Nafikiri ilikua nusu ya kiwango changu, kwani sikumbuki kama nilipoteza pasi labda nilikua nachelewa kupandisha timu kwa ajili ya uchovu kama alivyosema mwalimu ila hata mimi sijafurahishwa na kiwango changu cha jana kiukweli”

Vanessa, Ali Kiba washinda Tuzo Za Nzumari za Kenya
Mnyika Adai Tamisemi Kuamishiwa Ofisi Ya Rais Ni Mbinu Dhidi Ya Wapinzani