Ligi ya Taifa ya Wanawake inatarajiwa kuanza kesho Jumanne Novemba 1, 2016 katika viwanja sita kuchezwa, ambapo mchezo wa utafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kati ya wenyeji Baobao dhidi ya Victoria Queens ya Kagera.

Ligi hiyo ya kwanza kufanyika nchini Tanzania, lakini pia kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati imetokea kuvutia wadau kadhaa wakiwamo Azam Tv ambao wamedhamini kwa kuonyesha mubashara (live), michezo 30 itakayofanyika kweny viwanja mbalimbali kwa msimu mzima.

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwepo mawaziri na wabunge ambao kwa sasa wako kwenye vikao vya kamati mjini Dodoma, kwa pamoja wanatarajiwa kuwa katika hafla hiyo ambayo pilika pilika zake zinatarajiwa kuanza saa 8.00 mchana kabla ya mchezo kuanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

TFF imepeleka uzinduzi huo Dodoma ikiwa na lengo la kuhamasisha soka mikoani tofauti na Dar es Salaam ambapo ilizoeleka zaidi miaka ya nyuma kabla ya kuwa na mpango wa mashindano ya aina hiyo yanayoshirikisha timu 12 kutoka kona mbalimbali za nchi.

Mbali ya mchezo huo wa kundi B kati ya Baobao na Victoria, michezo mingine itakuwa ni kati ya Sisterz na Panama utakaofanyika Uwanja wa Tanganyika huko Kigoma wakati Marsh Academy ya Mwanza itacheza na Majengo Women ya Singida kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kundi A kutakuwa na michezo mitatu ambapo Viva Queens ya Mtwara itacheza na Mburahati Queens ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Fair Play ya Tanga itapambana na Evergreen ya Dar Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga huku JKT Queens ikiwa ni wenyeji wa Mlandizi Queens ya Pwani kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Koeman Amkaribisha Wayne Rooney Goodison Park
Rais Wa Armenia Ashindwa Kumuelewa Mourinho