Aliyekuwa kuwa Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Hitimana Thiery amejiunga na Klabu ya KMC FC ya Dar es salaam kama Kocha Mkuu.

Hitimana aliondoka Simba SC juma lililopita kwa makubaliano ya kuvunjwa kwa mkataba wake, baada ya kuhudumu klabuni hapo kwa miezi kadhaa, tangu alipoajiriwa mwanzoni mwa msimu huu 2021/22.

Leo Alhamis (Januari 06), Kocha huyo kutoka nchini Burundi amethibitishwa rasmi na Uongozi wa KMC FC kwa kusaini mkataba wa mwaka moja.

Hitimana atafanya kazi na Kocha mzawa Habib Kondo ambaye kwa kipindi kirefu amekua akikiongoza kikosi cha KMC FC kwenye michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

KMC FC inakua klabu ya nne kwa Hitimana kuitumikia nchini Tanzania baada ya kufanya kazi na klabu za Biashara United Mara, Namungo FC na Simba SC.

David Udoh kujaribiwa Simba SC
Nyoka wa kichawi asimamisha mradi wa Sh. 99 bilioni Tanga