Kocha msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Thierry Hitimana ameuomba radhi uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar kwa kile kilichotokea baina yake na viongozi wa klabu hiyo ya Morogoro.

Hitimana ambaye tayari ameshaanza kazi Simba SC amesema hana budi kuomba radhi kwa viongozi wa Mtibwa Sugar kutokana na kutambua kosa lake.

Amesema ujio wake hapa nchini ulisababishwa na Mtibwa Sugar ambao walimkamilishia kila kitu, lakini dakika za mwisho aliamua kutimkia Msimbazi.

“Kila kitu waligharamia wao mpaka nafika Tanzania ila baada ya kuanza mazoezi nao nikapigiwa simu na mabosi wa Simba wakinihitaji nikafanye kazi na Gomes, nikakubaliana nao kwa sababu ni mtu ambaye tumewahi kufanya kazi pamoja tukiwa Rayon Sports.”

“Mtibwa Sugar wana rasilimali nzuri ya wachezaji hivyo naamini kocha atakayekuja atafurahia na kufanya vizuri zaidi kwenye Ligi,” alisema huku akiwaomba yaishe wafungue ukurasa mpya kwani Mtibwa ni nyumbani kwake.” amesema Hitimana

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtibwa Sugar, Nassoro Abubakar alisema wamemsamehe kocha huyo huku wakimtakia kila la heri katika maisha yake mapya.

Rais Samia afanya uteuzi mwingine
Wachezaji wa Djibout wazamia Ufaransa