Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery amefichua siri ya kinachowasumbua wachezaji wake kwa sasa, na kuepelekea kushindwa kupata matokeo chanya.

Mtibwa Sugar ilipoteza mchezo wa hatua ya 32 kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kwa kufungwa na JKT Tanzania mwishoni mwa juma lililopita mjini Morogoro.

Mtibwa Sugar walipoteza mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju ya penati, baada ya kuazilisha sare ya 2-2, ndani ya dakika 90.

Kocha Hitimana ambaye alikabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha Mtibwa Sugar mwishoni mwa mwaka 2020, baada ya kuachana na Namungo FC amesema asilimia kubwa ya wachezaji wake bado wana tatizo la kukosa utimamu wa mweili (FIT), hivyo ana jukumu la kuifanyia kazi changamoto hiyo.

“Bado wachezaji hawajawa utimamu wa mwili ‘FIT’ katika mapambano ndani ya uwanja, jambo ambalo linafanya tumepoteza baadhi ya michezo iliyotukabili kwa siku za karibuni, nina kazi kubwa ya kuimaliza hii changamoto.”

“Ila haina maana kwamba hili tatizo litadumu, hapana, muda wake umekwisha ndio maana tunapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja. Kila kitu kinawezekana na ni muda wetu wa kurejea kwenye ubora wetu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa.” amesema Hitimana

Kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 23 huku ikiwa imesashuka dimbani mara 19.

Museveni awapuuzia Facebook
Simba SC kuifuata Al Merrikh