Ndege ya EgyptAir, inayotambulika kama Flight 804 imepotea ghafla angani ikiwa na watu 66 wa mataifa mbalimbali muda mfupi uliopita.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Jijini Paris nchini Ufaransa kuelekea jijini Cairo nchini Misri, imepotea kwenye rada pamoja na mawasiliano yote hivyo kutobainika ilipo.

Kwa mara ya mwisho ilionekana ikiwa inaambaa juu ya bahari ya Mediterranean, umbali wa futi 37,000 kutoka usawa wa bahari.

Ndugu na jamaa wa watu waliokuwa kwenye ndege hiyo wamekusanyika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cairo kwa lengo la kupata habari zozote kuhusu wapendwa wao.

Jeshi la Maji la Misri limeanza msako mkali wa ndege hiyo likishirikiana na jeshi la maji la Ugiriki.

Chanzo: CNN

Tanzania Itasafa Sana Kuongezewa Uwakilishi CAF
Watatu Ama Wanne Kuongeza Nguvu Leicester City - 2016-17