Mbunge wa Singida Magharibi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Elibariki Kingu ameahidi kumlinda Rais Dkt. John Magufuli kwa gharama yeyote ile kwasababu wanajua nia na dira ya wapi analipeleka taifa.

Amesema kuwa wao kama wabunge wa CCM wapo tayari kushughulika na chokochoko zinazofanywa na watu mbalimbali zenye lengo la kuathiri utendaji kazi wa kiongozi huyo.

“Tutahakikisha mwenendo salama unaolinda heshima ya Rais ndani ya bunge na nje ya bunge, Chokochoko za upinzani ziko ndani ya uwezo wetu. Mh. Rais fanya kazi kwa ukitambua uko mbele yetu wewe na nyuma yako tupo sisi.”amesema Kingu

Hata hivyo, Kingu amesema kuwa Rais Magufuli anatakiwa kulindwa kwa sababu amefuta aibu kubwa ambayo ilikuwa imelikumba taifa ikiwa ni pamoja na kufufua shirika la ndege (ATCL).

 

Nigeria kutoa tiba ya bure kwa wananchi wake
Mama ajinyonga baada ya kuua wanawe wanne

Comments

comments