Watu wengi waishio maeneo yenye joto kama Dar es salaam huwa hawapendelei kutumia kinywaji cha chai kutokana na kinywaji hiko kuchochea ongezeko la joto na utokaji mwingi wa jasho, wengi wao hupendelea kunywa juice au soda kama chai kukata kiu yao, Leo nakuletea faida za kwa nini unywe chai ya kahawa angalau mara moja kwa siku.

Wataalamu wamechambua faida saba anazozipata mtu anayetumia kinywaji cha chai, japo kumekuwa na minong’ono inayosema kahawa husababisha magonjwa ya moyo, hilo linawezekana endapo masharti ya kiungo hiko yakivunjwa, Kiasi kikubwa cha kahawa kwenye chai hupoteza radha ya kinywaji hiko kwa kukifanya kiwe kichungu, hivyo hakikisha unafanya matumzi sahihi ya kiungo hiki katika chai.

Hizi hapa sababu saba kwanini utumie chai ya kahawa kwa afya yako.

  1. Kahawa huchangamsha akili yako, kama upo kazini unaweza kujikuta unasinzia au kupatwa na uchomvu, utumiaji wa chai ya kahawa husadia kuchangamsha mwili pamoja na akili yako ili kuimarisha ufanisi wa kazi, kahawa ina glucose ambayo husaidia kuongeza nguvu katika mwili
  2. Kahawa husaidia kufanya sawa msukumo wa damu katika mwili.
  3.  Kahawa husaidia mwili kujikinga na magonjwa kwa kuzipa nguvu chembe chembe za mwili zinazokinzana na magonjwa mwilini kwani kahawa huupa nguvu mwili na kuufanya upambane vyema na magonjwa na kukinga mwili dhidi ya magonjwa hasa kansa
  4. Kahawa husaidia kupunguza maumivu ya kichwa, hivyo baada ya kutumia panadol, au Headex inashauriwa utumie kiwango kikubwa cha maji au chai ya kahawa kuponya maumivu ya kichwa.
  5. Kahawa hupunguza msongo wa mawazo kwani inamiliki homini inayojulikana kama Dopamine na Seratonin ambayo inasaidia kukuchangamsha na kupunguza msongo wa mawazo kwenye ubongo wako
  6. Kahawa huongeza uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vitu kwani kahawa hukupa nguva ya kujifunza zaidi na kukumbuka mambo kwa ufasaha zaidi.
  7. Kahawa husaidia kupunguza uzito wa mwili kwani hupunguza hamu ya kula kwa muda mfupi.

Kwa faida hizo ni jinsi gani utaona umuhimu wa kutumia kinywaji cha chai ya kahawa katika siku yako ili iweze kwenda vizuri.

Leo kumbukumbu ya miaka 37 kifo cha Bob Marley
Nchi hii inatia aibu kuagiza mafuta nje ya nchi- Zitto Kabwe

Comments

comments